Saturday, 18 January 2014

4 wafariki Misri katiba mpya ikisakwa


Polisi waliwakamata baadhi ya waandamanaji mjini Cairo
Waziri wa afya nchini Misri amesema kuwa idadi ya watu waliofariki katika ghasia za kisiasa wakati kura ya maamuzi kuhusu katiba mpya ilipokuwa inaendelea imefika watu 4.
Watu wengine 15 walijeruhiwa katika ghasia hizo za Ijumaa.
Wamisri wanasubiri matokeo ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo yatarajiwa kutangazwa baadaye Jumamosi.
Ghasis hizo zilianza baada ya wafuasi wa aliyekuwa Rais wa Misri Mohammed Morsi kuandamana mjini Cairo, na katika mikoa mingine wakilaani rasimu ya katiba inayopigiwa kura.
Polisi walilazimika kufyatua gesi ya kutoa machozi hewani ili kuwatawanya waandamanaji hao ambao hawakuwa na kibali cha kuwaruhusu kuandamana.
Tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa mamlakani Morsi mwezi Julai, wanaharakati wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, wamekuwa wakizusha zogo, kuipinga serikali ya mpito wakisema kuwa sio halali.
Taarifa za awali zilisema kuwa 90% ya watu walishiriki kura hiyo ya maamuzi
(Chanzo BBC).

No comments:

Post a Comment